Kila kitu tunachopanga kufanya, kinawezekana.

ATD Fourth World
Stories of Change
Published in
3 min readSep 20, 2018

--

Na Jean Venard

Tovuti ya harakati za Kimataifa za ATD Dunia ya Nne, inaeleza hadithi zinazoonyesha kuwa umasikini unaepukika na kwamba pamoja tunaweza kuuzuia umasikini. Jean Venard, mfanyakazi wa kujitolea kwa muda wote na mjumbe aliyepita wa Ukanda wa Afrika alieleza hadithi ya Reuben, mwanachama wa ATD dunia ya nne nchini Tanzania.

Katika kijiji cha Kusini Magharibi mwa Tanzania, Reuben, mwanachama wa ATD Dunia ya Nne, ni mfano hai wa maendeleo yaliyojikita katika ufahamu wa wakazi na uwezo wao wa kuunganisha nguvu pamoja.

Sehemu ya ari ya Reuben katika kupambana na umasikini bila shaka inatokana na ujuzi wake binafsi. Anakumbuka wakati alipokuwa kijana, watu wote waliokuwa wakirejea kutoka Dar es Salaam, jiji kubwa linalopakana na bahari, lenye umbali wa masaa kumi na mbili kutoka kijijini kwake Reuben, ambao walikuwa wakisema kuwa kila kitu huko kilikuwa kizuri. Siku moja aliondoka pia kwemda kwenye jiji hilo kubwa na akaishia kufanya kazi ngumu kama kibarua katika maeneo ya ujenzi kwa malipo ya shilingi mia tatu za kitanzania kwa siku, kiasi kwamba ikawa ngumu kulipia chakula chake cha jioni.

Akaamua kusonga mbele. Akawa hali chakula kila siku ya tatu, ili aweze kununua tiketi ya kucheza bahati nasibu. Je, angeweza kuwa mshindi wa shilingi milioni iliyokuwa zawadi kuu? Ama zawadi ya pili ya nusu milioni? Au hata kama ya tatu ya shilingi laki mbili na hamsini elfu?

Kwa bahati mbaya, tiketi zake zote tatu hazikushinda! Akabaki amekata tamaa na kuendelea kushangaa kwa nini yeye hakuwa mshindi? Akaiangalia mashine ya bahati nasibu iliyomkatalia kuwa mshindi. Akaendelea kuiangalia sana kiasi cha kubaki na umbo lake kichwani, kuifanya kuwa halisi kwake. Baada ya muda, alichukua umbo la mashine lililoko kichwani na kuijenga mashine halisi, na ikafanya kazi!

Polisi aliyegundua kuhusu hili na ilimshtusha mno kiasi cha kuona kuwa Reuben ana akili sana na akaamua kumpa fedha badala ya kumtoza fine kwa kuandaa michezo haramu ya Kamari!

Reuben alipata fedha kutokana na mchezo wake wa bahati nasibu lakini mwishowe hakuwa na furaha. “Sikujisikia vizuri kupata fedha kupitia migongo ya watu wengine”

Alijifunza kitu kimoja kupitia mapito yake: aliamini kuwa vijana wote ili kuondokana na umasikini, walihitaji kitu kimoja- ujuzi au mafunzo Fulani. Katika familia yao, wote walikuwa wafua vyuma, hivyo akaamua kurudi katika hiyo biashara. Akaihamasisha jumuiya Fulani iliyoanzishwa na kaka yake, (Kisangani Smith Group) na kuanzisha sehemu ambapo vijana wanaweza kufundishwa. Wakajifunza biashara hapo, wakitengeneza zana za kilimo maeneo jirani na wakulima.

Mmoja wao, Damian, alisema, “nilitaka kusoma na nikamuuliza Reuben kama ningeweza kufanya hivyo, akanitia moyo. Nikafanikiwa kwenda shule huku nikafanya kazi kama mfua vyuma ili niweze kujilipia masomo yangu. Elimu ni ufunguzi wa fikra na uhalisia mwingine.

Reuben na kikundi chake, tokea 1998 wameanzisha mradi wa upandaji miti tena katika maeneo inapokatwa kwa lengo la kufanya uuzaji na usambazaji wa mbao. Wanakikundi wa Kikundi cha wafua vyuma Kisangani (Kisangani Smith Group) wanafanya kazi kutokana na ujuzi wanaoupata kutokana na kuwatazama wengine wafanyavyo wanapokuwa kazini. Hiyo pia iliwasaidia kuuangalizia mfereji mdogo na kuugeuza ili kutengeneza mfumo wa umwagiliaji asilia kwaajili ya shule ya chekechea ya eneo lao. Pia, bila kusubiri msaada wa serikali ambao hupitia hatua ndefu, wanakikundi waliamua kuchukulia masuala mikononi mwao na kutengeneza umeme unaotumia nishati ya maji.

Mradi huu wa maendeleo kwa jamii ulitokana na duka la wafua vyuma lililolenga kuwafundisha vijana. Kwa Reuben, ilikuwa kawaida kuwa kila mtu kijijini alihusishwa na kwamba waliamini kila mtu angefaidika na mradi huu. Kuna mambo mawili muhimu yaliyopelekea mafanikio hayo: uwezo wa kubuni kitu cha kiufundi kwa kutumia ujuzi asilia, kwa upande mwingine; na wakati huohuo, uwezo wa kuunganisha nguvu katika kutekeleza mradi huo.

Pamoja na Reuben kufahamu umuhimu wa kuunganisha nguvu, anamaliza kwa kusema: “ Kupitia ATA Dunia ya Nnne, nimepata hamasa na ujasiri niliouhitaji. Nimeelewa kuwa, asante kwa umoja na mshikamano, kila kitu tulichopanga kufanya kinawezekana.”

--

--

Eradicating global poverty & exclusion through inclusive participation. #StopPoverty